Skip to main content

Swahili

Karibu katika shule ya mtandaoni ya Karense kupitia tovuti yake ya NoTe Norwegian Teaching.Mafunzo hutolewa kwa lugha ya kinorwegian katika ngazi zote. Na kozi zetu zinakuandaa kwa ajili ya kufanya testi ya lugha na Bergentesti(kiwango cha juu cha lugha).Na imethibitishwa/kuidhinishwa na inatambuliwa  na UDI pamoja na  Kompetanse Norge.Kozi zote zinatolewa na waalimu wenye uzoefu na waliobobea na  ambao lugha hii ni lugha mama kwao. Na ambao wamekuwa wakitoa mafunzo ya lugha hii  kwa muda mrefu na  katika njia tofauti.

Urahisi wa kozi za mtandaoni

Kozi zetu ni kwa njia ya mtandao na hivyo zina urahisi.Unaweza kusoma kwa wakati unaotaka wewe na mahali popote ulipo.Kozi zetu zinawezekana kwa watu  wote na katika mazingira yeyote,hata kama uko bize na unafanya kazi sana, ama uko nyumbani ama ni mwanafunzi unasoma.

Tunatoa kozi katika ngazi ya A1, A2, B1, B2 na C1.Kwahiyo unaweza kuchagua kozi ikiwa unaanza au tayari unayo kiwango cha juu cha lugha na unataka kujiendeleza zaidi.Tunashauri  masaa 2-3 ndani ya  muda wa  kazi kila siku kutumika kwa ajili ya kozi.

Tunatoa pia kozi za afya na za chekechea kwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya afya na chekechea.Kwa kuongezea, tunayo pia mafunzo ya namna ya kuzungumza kinorwegian na mbao wanataka kuboresha namna ya kuzungumza lugha hii.Kwa wale ambao wataenda kozi ya sayansi jamii(sammfunnskunnskapskurs ) masaa 50,tunatoa mafunzo haya kwa lugha ya kinorwegian, kiarabu na kiingereza.

 Shule ya mtandaoni ilianzishwa mnamo mwaka 2015.  Karense ambae ni mwalimu  ametumia uzoefu wake wa zaidi ya miaka 15 aliyokuwa anafundisha kama mwalimu wa lugha kutengeneza kozi hii ambayo  imeleta matokeo mazuri.Shule hii kupitia mtandaoni ina timu nzima ya waalimu waliofuzu mafunzo kutoka Norway  ambao wanawasaidia wanafunzi wetu.Kupitia kozi zetu za kwenye mtandao unaweza kuwa na fursa ya rasilimali zetu kama vile video za mwalimu Karense za kwenye You-Tubes,ujumbe wa sauti,akaunti ya instagram na kikundi cha facebook.

Kozi zilizopo na mwongozo wa kibinafsi

Kozi za lugha ya kinorwegian zitolewazo mtandaoni ni pamoja na kusoma, kusikiliza, kuandika na rekodi za sauti. Mazoezi ya uandishi ambayo yanawasilishwa, yanasomwa, yanasahihishwa na yanakaguliwa na walimu wetu. Hapa kuna vidokezo juu ya namna ya kuifanya bora zaidi wakati ujao.

Soma zaidi juu ya kila kozi kuona kile kilichojumishwa au tutumie barua pepe.

Pia inajumuisha lisaa limoja kuzungumza na mwalimu kwa mwezi kwenye kozi. Masaa haya yanaweza kutumika katika mafunzo ya kuzungumza. Ambapo  unaweza kuboresha matamshi yako (namna ya kutamka maneno),na kuwa mjuzi katika kuzungumza lugha ya kinorwegian, sio tu katika kuandika na kusoma.Unaweza kutumia pia huo muda katika kupitia sarufi(gramatikk)ambazo una tatizo nazo na kujiandaa pia utakapokuwa kwa mfano kwenye mahojiano ya kazi.

Tazama kozi yetu hapa.

Baada ya masaa hayo pia, utapokea repoti ya maandishi ama mazungumzo zenye kuonyesha vitu ulivojifunza, maneno ambayo unatakiwa kuyafanyia mazoezi na utapata linki ambayo itakusaidia katika kijifunza kwako.    

Kozi ya kingereza katika ngazi zote

NoTe pia inatoa kozi katika ngazi zote, na pia kozi ya kingereza cha kukusaidia katika biashara.Tuna kozi za mtandaoni kuanzia mwezi 1-6, na kiwango cha B1.Na pengine kama unataka kiwango cha juu zaidi baada ya kumaliza kozi,unaweza kuagiza masaa zaidi kutoka kwa mwalimu.

Kozi ya kingereza sio tu kwa wale wanaotaka kuijua kwa mawasiliano,lakini pia ni kwa wale ambao  wanahitaji kujiandaa na mtihani  wa TOEFL au IELTS kwa ajili ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu  nje ya nchi.Walimu wetu wa kozi ya kingereza asili yao ni  wamarekani ila wanaishi Norway.

Kutana na Karense

Kwenye chaneli ya YouTube unaweza kujifunza kutoka kwa Karense.Na utapata kujionea kozi zetu  mtandaoni.Tazama video hii kujionea namna kozi zetu zilivyo.

Jiandikishe

Tunatarajia kuona wanafunzi wapya kwenye kozi zetu.Tunawakaribisha  watu wote , haijalishi una kiwango gani cha lugha na unaenda wapi.Malengo yetu ni kukufanya wewe uwe bora katika lugha .